Usiku  wa Arubaini ya Imam Hussein (as) si tu ni kumbukumbu ya huzuni, bali pia ni mlipuko (uongezekaji) wa imani, mshikamano, na mapenzi ya dhati na ya haki kwa Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w), Al-Imam Al-Hussein (as). Karbala, kwa mara nyingine tena, imekuwa kitovu cha umma wa Kiislamu duniani.

18 Agosti 2025 - 14:56

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mamilioni ya Waumini kutoka kona zote za dunia wamefika katika Mji Mtukufu wa Karbala ili kuadhimisha usiku wa Arubaini wakiwa karibu zaidi na kaburi takatifu la Bwana wa Mashahidi – Imamu Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Habari Pichani | Usiku wa Arubaini Huko Karbala: Kilele cha Shauku na Mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s) – Sehemu ya 1

Ripoti hii kupitia picha hizi inaangazia mazingira ya kiroho yaliyotanda Karbala, mikusanyiko mikubwa ya Mahujaji (Mazuwwari), na upendo usio na kifani waliouonyesha kwa Sayyid al-Shuhada (a.s). Kila kona ya Haram imejaa machozi, dua, na nyoyo zilizojaa mapenzi kwa mwana wa Sayyidat Fatima Al-Zahraa(a.s).

Usiku  wa Arubaini ya Imam Hussein (as) si tu ni kumbukumbu ya huzuni, bali pia ni mlipuko (uongezekaji) wa imani, mshikamano, na mapenzi ya dhati na ya haki kwa Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w), Al-Imam Al-Hussein (as). Karbala, kwa mara nyingine tena, imekuwa kitovu cha umma wa Kiislamu duniani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha